NAHODHA wa kikosi cha ubingwa wa Kombe la Dunia Argentina, Diego Maradona ameanzisha vita ya maneno na Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Sepp Blatter jana akisema babu huyo wa miaka raia wa Uswisi ameifikisha soka 'pabaya'.
Huku ukiwa umebaki mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wa FIFA, Maradona, mmoja wa wachezaji wakubwa kuwahi kutokea duniani na aliyekuwa chachu ya ushindi wa Argentina Kombe la Dunia mwaka 1986, amesema muda umefika sasa Blatter aondoke.
Amesema atafanya yote awezayo kumsaidia Prince Ali Bin Al Hussein kushinda uchaguzi huo, ingawa pia raia huyo wa Jordan mwenye umri wa miaka 39 alisema jana anaweza kufikiria kujitoa iwapo ataona mmoja kati ya wagombea wengine wawili anaweza kushinda.
Gwiji wa Argentina, Diego Maradona (kulkia) amamfanyia kampeni Prince Ali Bin Al Hussein
Akizungumza wakati wa mahojiano na Guillem Balague, katika Mkutano wa Soccerex bara la Asian kwenye ukumbi wa King Hussein Centre, kiasi cha kilomita 60 kugoka mji mkuunwa Jordan, Amman, Maradona alimshambulia Blatter na akamfagilia mtoto wa Mfalme wa Jordan.
Maradona, mwenye umri wa miaka 54, ambaye alichaguliwa kwa pamoja na Pele kama wachezaji bora wa Karne ya 20 na FIFA mwaka 2000, amesema anaamini kuendelea kwa Blatter, anayewania Urais wa kwa mara ya tano ni 'mbaya' kwa soka.
"Amefanya madhara mengi katika soka tangu amekuwa hapo. Ni wakati wa yeye kung'atuka na kutuacha sisi, ambao tuna nguvu za kutosha kuisuka upya soka,"amesema Maradona.
0 comments:
Post a Comment