TIMU za JKT Tanzania na Mashujaa zimegawana pointi kwa sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
JKT Tanzania inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 13 nafasi ya nane, nyuma ya Mashujaa FC yenye pointi 19 za mechi 14 nafasi ya saba.
0 comments:
Post a Comment