Tetesi za J'tatu magazeti ya Ulaya

DROGBA ATEMWA CHELSEA, ANAKWENDA CHINA...

MKONGWE Didier Drogba mwenye umri wa miaka 34, ni kama tayari amekwishapiga mpira wake wa mwisho Chelsea, na klabu hiyo inatarajia atathibitisha uhamisho wa bure kwenda Shanghai Shenhua ya China.
KIUNGO wa Tottenham, Luka Modric mwenye umri wa miaka 26, anatarajia kuomba uhamisho baada ya klabu hiyo kukosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Didier Drogba
Didier Drogba 
KOCHA wa West Ham, Sam Allardyce anataka kumrejesha kiungo wa zamani wa Hammer, Joe Cole mwenye umri wa miaka, 30, arejeshe cheche zake Upton Park baada ya klabu hiyo kurejea Ligi Kuu. Msimu uliopita Cole alikuwa akicheza kwa mkopo Lille ya Ufaransa, akitokea Liverpool.
NYOTA wa Blackpool, Matt Phillips mwenye umri wa miaka 21, bado anaweza kucheza Ligi Kuu msimu ujao, licha ya timu yake kushindwa kupanda, baada ya kunaswa na jicho la kocha wa Reading,Brian McDermott.

MANCINI MIAKA MITATU ZAIDI MAN CITY

KLABU ya Manchester City inatarajiwa kumzawadia mkataba wa miaka mitatu kocha wao Roberto Mancini utakaokuwa na thamani ya pauni Milioni 15.
WACHEZAJI wawili wa Tottenham, Louis Saha na Steven Pienaar wamekandiwa na mashabiki wa timu yao kwa kitendo chao cha kuwapongeza Chelsea kwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
KOCHA wa Ajax, Frank de Boer ndiye ni mtu namba moja kwa sasa katika orodha ya makocha wanaowaniwa Liverpool kuziba nafasi ya Kenny Dalglish aliyefukuzwa.
MMILIKI wa Chelsea, Roman Abramovich anataka mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na a metoa hotuba kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya ushindi wa mikwaju ya penalti dhidi ya Bayern Munich.
Roberto Mancini set to be offered a new deal
Mancini 
KOCHA wa Muda wa Chelsea, Roberto Di Matteo ghafla amegeuka lulu na klabu ya Aston Villa inamtaka baada ya kuwapa Chelsea taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
WACHEZAJI wamemtaka mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kumfanya Roberto Di Matteo awe kocha wao kamili, baada ya kuwaongoza vema kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
NYOTA wa Ivory Coast, Salomon Kalou anaamini Chelsea isingeweza kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kama Andre Villas-Boas angebaki kuwa kocha wa Stamford Bridge.
OBI MIKEL ALIMTILIA GUNDU ROBBEN
KIUNGO wa Chelsea, John Mikel Obi amesema alimuambia Arjen Robben atakosa penalti, wakati mchezaji huyo wa Bayern Munich akijiandaa kupiga mkwaju huo katika dakika za nyongeza.