• HABARI MPYA

    Thursday, May 17, 2012

    MAN CITY YAFANYA KUFURU KWA IBRAHIMOVIC


    Zlatan Ibrahimovic
    TOP TARGET ... Zlatan Ibrahimovic
    Last Updated: 17th May 2012

    MANCHESTER CITY imetenga dau la pauni Milioni 25 kwa ajili ya mshambuliaji wa AC Milan, Zlatan Ibrahimovic.

    Kocha Roberto Mancini atampa Msweden huyo mshahara wa pauni 300,000 kwa wiki.
    Hiyo dhahiri itamfanya awe mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika Ligi Kuu ya England, akimpiku kiungo wa City, Yaya Toure anayelipwa pauni250,000 kwa wikki.
    Lakini huwezi kuamini eti Ibrahimovic, mwenye umri wa miaka 30, ameomba muda kuifikiria ofa hiyo.
    Hii ni mara ya pili kwa Mancini kujaribu kumsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona, Juventus na Inter Milan atue  Eithad na safari hii anatarajia kufanikiwa.
    Mancini alimsajili Ibrahimovic wakati akiwa Inter Milan kwa pauni Milioni 22 mwaka 2006.
    Na sasa yuko tayari kubomoa beki kumnasa ngongoti huyo mwenye urefu wa futi 6 na inchi 5 kwa dau tamu la usajili, posho kibwenana marupurupu mengine kibao — sambamba na mshahara mkubwa kwa wiki.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY YAFANYA KUFURU KWA IBRAHIMOVIC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top