• HABARI MPYA

    Thursday, May 17, 2012

    TEVEZ AMUAMBIA FERGUSON; "USIJIONE RAIS WA ENGLAND"


    Carlos Tevez
    SIOMBI MSAMAHA ... Carlos Tevez
    EXCLUSIVE
    Published: 16th May 2012

    CARLOS TEVEZ ameanzisha rasmi vita ya maneno na kocha wake wa zamani, Alex Ferguson — akimuambia: “Unafikiri wewe ni rais wa England.”

    Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City alibeba bangto lililoandikwa ‘RIP Fergie’ wakati sherehe za klabu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England Jumatatu wiki hii.
    City iliomba radhi kwa kitendo hicho cha Tevez, lakini Muargentina huyo amegoma kusema samahani.
    Alisema: “Inaonekana kama Ferguson ni rais wa England.
    “Wakati wote anazungumza mambo yasiyo na maama juu yangu na sijawahi kumuambia aniombe msamaha.
    “Wakati mtu mmoja anapomtania mwingine pia, unaweza kuomba radhi. Lakini siwezi kusema swamahani.”
    Bango alilobeba Tevez kwa mashabiki, ilikuwa ni kukumbushia kauli ya Ferguson kabla ya mechi ya wapinzani hao wa jiji la Manchester mwaka 2009.
    Aliulizwa kama itafikia Man United watakuwa vibonde wa City, Ferguson akasema: “Siyo nikiwa hai,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TEVEZ AMUAMBIA FERGUSON; "USIJIONE RAIS WA ENGLAND" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top