Published: 16th May 2012
ROBIN VAN PERSIE sasa yuko mguu nje, mguu ndani Arsenal- baada ya mazungumzo ya jana kati yake na kocha Arsene Wenger kumalizika bila kufikia mwafaka.
The Gunners walitumaini kumtuliza kwa mkataba mpya wa mika mitatu ambao ndani yake walimuandalia mshahara wa pauni 130,000 kwa wiki ambao walidhani ungemfanya apuuze ofa mabingwa wapya wa Ligi Kuu, Manchester City na kubaki Emirates.
Lakini mazungumzo ya jana, yalivunjika bila makubaliano.
Shaka imetawala sasa kwamba Van Persie anaweza kuondoka Arsenal na kuhamishia cheche zake Etihad, huku ikielezea kiu yake ya wazi wazi ya kumnasa mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu.
Habari zilizopatikana jana zimesema kwamba, Arsenal iko tayari kucheza ngoma ngumu iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, Van Persie hataki kubaki ba watamlazimisha amalizie mwaka wake mmoja uliobaki katika mkataba wake wa sasa.
Mholanzi huyo aliyeifungia mabao 37 The Gunners msimu huu katika Ligi Kuu, ameshinda tuzo za Mwanasoka Bora wa Mwaka ya PFA na Waandishi wa Soka.
0 comments:
Post a Comment