• HABARI MPYA

    Thursday, June 07, 2012

    GAMBIA WAJA NA NGE 11 WA ULAYA KUIVAA STARS JUMAMOSI


    TIMU ya soka ya taifa ya Gambia, The Scorpions inatarajiwa kuwasili leo usiku saa 3:20, kikosini ikiwa na wachezaji 11 wanaocheza soka ya kulipwa nchi mbalimbali Ulaya.
    Wachezaji wa kulipwa wa Gambia watakaotua na ndege ya Kenya Airways tayari kwa mechi ya Kundi C dhidi ya wenyeji Tanzania, Taifa Stars Jumamosi kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia ni; Momodou Futty Danso wa Portland Timbers ya Marekani, Lamin Basmen Samateh wa Hibernian F.C. ya Scotland, Pa Saikou Kujabi wa NK Lokomotiva ya Croatia, Mustapha Kebba Jarju wa Mons ya Ubelgiji, Yankuba Mal Ceesay wa Djurgardens IF ya Sweden,
    Demba Savage wa HJK ya Finland, Alieu Darboe wa Le Mans ya Ufaransa, Momodou Ceesay wa MSK Zilina ya Slovakia, Pa Modou Jagne wa FC St. Gallen ya Uswisi, Tijan Jaiteh wa Randers FC ya Denmark na Omar Colley wa NK Triglav ya Slevenia.
    Wengine ambao wanacheaa nyumbani ni Musa Camara, Abdou Jammeh, Ousman Koli, Saihou Gassama, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa, Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe na Saloum Faal.
    The Scorpions ilipaswa kubadili ndege Dakar, Senegal jana usiku lakini kukawa na ucheleweshaji (delay), hivyo ikashindwa kuwahi Nairobi, Kenya ambapo ingeunganisha kwa ndege ya alfajiri kuja Dar es Salaam.
    Timu hiyo itafikia kwenye hoteli Sapphire iliyopo Mtaa wa Lindi na Sikukuu eneo la Kariakoo, wakati waamuzi kutoka Zimbabwe ndiyo watakaochezesha mechi hiyo.
    Refa atakuwa Ruzive Ruzive na wasaidizi wake watakuwa ni Salani Ncube na Edgar Rumeck,  mwamuzi wa akiba ni Norman Matemera na Kamisaa ni Fanie Wallace Mabuza kutoka Swaziland wakati mtathmini wa waamuzi ni Ali Baligeya Waiswa.
    Waamuzi hao watawasili nchini kesho (Juni 8 mwaka huu) saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways wakati Kamishna wa mechi hiyo atawasili siku hiyo hiyo saa 12.50 jioni kwa ndege ya South African Airways na Mtathmini wa waamuzi atatua pia Juni 8 mwaka huu saa 7.55 mchana kwa ndege ya Kenya Airways.
    Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaendelea na mazoezi leo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen.

    PROGRAMU YA MAZOEZI YA GAMBIA
    IJUMAA JUNI 8
    01.00 asubuhi Mazoezi- Uwanja wa Karume
    10.00 jioni   Mazoezi- Uwanja wa Taifa

    JUMAMOSI JUNI 9
    04.00 asubuhi  Mkutano na Waandishi wa Habari- Ukumbi wa TFF
    10.00 jioni  Mazoezi- Uwanja wa Taifa
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GAMBIA WAJA NA NGE 11 WA ULAYA KUIVAA STARS JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top