• HABARI MPYA

    Thursday, June 07, 2012

    MAN CITY HATARINI KUMPOTEZA MANCINI


    Roberto Mancini
    JUKUMU LA KITAIFA ... Roberto Mancini
    EXCLUSIVE
    Last Updated: 07th June 2012

    MANCHESTER CITY inaweza kujikuta katika inampoteza kocha wake, Roberto Mancini kutokana na nchi yake, Italia kutaka kumpa jukumu la kitaifa.

    Kocha wa sasa wa The Azzurri, Cesare Prandelli yuko kwenye shinikizo kali na matokeo yoyote mbaya katika Euro 2012 yatamfanya afukuzwe kazi.
    Na Mancini, mwenye umri wa miaka 47, ndio mtu anayekubalika zaidi na FA ya Italia kumbadili Prandelli, baada ya kutwaa ndoo ya Ligi Kuu ya England.
    Bosi huyo wa City, amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake Etihad. Mjadala kuhusu mkataba mpya umekwishafanyika, lakini bado hajasaini.
    Mancini kwa sasa yupo mapumzikoni Sardinia ambako atakuwapo hadi wakati wa maandalizi ya msimu mpya mwezi ujao.
    Mtaliano huyo amesema angependa kuikochi nchi yake siku moja, ingawa hakutarajia nafasi hiyo ingekuja mapema kiasi hiki.
    City itasaini mkataba mpya na kocha huyo wa miaka minne , ambao utapandisha mshahara wake kutoka pauni Milioni 3.5 hadi Milioni 5.5 kwa mwaka.
    Hiyo itamfanya awe kocha anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika Ligi Kuu ya England, sambamba na kocha wa Manchester United, Alex Ferguson.
    Kocha huyo wa zamani wa Inter Milan amefanya kazi nzuri katika kipindi cha miaka miwili na nusu akiwa na City.
    KatikaIn his first full season he won the club their first trophy in 35 years with the FA Cup. Then last term he delivered City’s first title in 44 years
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY HATARINI KUMPOTEZA MANCINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top