• HABARI MPYA

    Thursday, June 07, 2012

    RAGE AWASHITAKI YANGA FIFA, AWAITA WAHUNI, WANAHARIBU SOKA

    Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage akizungumza na Waandishi wa Habari, mchana huu makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi kuhusu sakata la Yondan
    MWENYEKITI wa klabu ya Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage amesema atawashitaki wapinzani wao wa jadi, Yanga, Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kwa kitendo chao cha kumsajili beki wao, Kelvin Patrick Yondan wakati bado ana makataba na klabu yake.
    Rage amesema leo mchana katika Mkutano na Waandishi wa Habari, makao makuu ya Simba, Mtaa wa Msimbazi kwamba ushahidi wa Yanga kumsajili Yondan wakati amekwishasaini Simba, ni picha anayoonekana akisaini wakati amevaa jezi mpya ya timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars yenye nembo ya wadhamini wapya, Kilimanjaro Beer.
    Rage amesema kwamba kitendo walichofanya Yanga ni uhuni ni kinautia aibu mchezo wa soka, hivyo amewaagiza mawakili wa klabu hiyo kukaa leo kuandaa mashitaka ya kupeleka FIFA.
    Aidha, Rage alionyesha nakala ya mkataba ambao Simba imesaini na Yondan, ikionyesha amepeaa fedha taslimu Sh. Milioni 25 kwa miaka miwili.
    “Simba Sports Club imesikitishwa na kitendo cha Young Africans kuvunja taratibu za usajili kwa kumrubuni mchezaji wake Kelvin Patrick Yondan, kwanza kwa kuzungumza naye na baadaye kwa ushahidi wa picha kuonekana wakimuandikisha makaratasi ambayo baadaye imeripotiwa na vyombo vya Habari kwamba alikuwa akisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo ya Young Africans,” alisema Rage.
    Nakala za mkataba wa Yondan na Simba SC


    Alisema Yondan ni mchezaji halali wa Simba SC aliye na mkataba hadi Mei 31, mwaka 2014, baada ya kuongeza mkataba na klabu yake, Desemba 23, mwaka jana. Mkataba wa awali wa Yondan Simba uliisha Mei 31, mwaka huu. “Sheria za FIFA za hadhi na uhamisho wa wachezaji ziko wazi, katika kipengele cha 5 kifungu kidogo cha 2 kinasema kwamba mchezaji atasajiliwa kuichezea timu moja tu kwa wakati mmoja,”alisema Rage.
    Mapema jana BIN ZUBEIRY 'ilifichua' Yondan kusaini Yanga kwa Sh. Milioni 30, mkataba wa miaka miwili- maana yake mchezaji huyo amekunja zaidi ya Sh. Milioni 55 kwa mikataba yote.
    Lakini Yondan mwenyewe jana aliukana mkataba wa Simba, akisema hajasaini. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAGE AWASHITAKI YANGA FIFA, AWAITA WAHUNI, WANAHARIBU SOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top