• HABARI MPYA

    Wednesday, June 13, 2012

    RASMI; DAMAYO AANGUKA MIAKA MIWILI JANGWANI JION HII

    HATIMAYE klabu Yanga ya Dar es Salaam, leo imefanikiwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili, kiungo mkabaji wa JKT Ruvu ya Pwani, Frank Damayo (pichani kushoto) anayechezea timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
    Yanga imezipiga bao Simba na Azam FC, ambazo pia zilikuwa zinawania saini ya chipukizi huyo. Zoezi hilo limefanikishwa jioni ya leo kwa jitihada za pamoja za Seif Ahmad 'Magari' na Abdallah Ahmad Bin Kleb jioni hii.
    "Tumemalizana na Damayo, tumesaini naye mkataba wa miaka miwili jioni hii,"alisema Seif kuiambia BIN ZUBEIRY. Jana kutwa nzima Yanga walikuwa wanakwenda mbio kusaka saini ya mchezaji huyo na haimaye wamefanikiwa leo. Seif amesema kabla ya kuzungumza na mchezaji huyo, walianza kwanza kuzungumza na klabu yake, ikawaruhusu kufanya naye mazungumzo.
    Damayo alicheza soka ya maana katika mechi ya Jumapili ya Taifa Stars na Gambia, Kundi C kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil. Katika mechi hiyo, ambayo Stars ilishinda 2-1, Damayo alicheza kwa maelewano makubwa na beki Kelvin Yondan wa Simba, ambaye pia amesaini Yanga- ingawa na klabu yake inasistiza ina mkataba naye.
    Pamoja na Damayo, Yanga pia imemsajili chipukizi wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Simon Msuva. Wengine ambao tayari wamekwishasajiliwa Yanga ni kipa Ally Mustafa 'Barthez', beki Kelvin Yondan wote kutoka Simba, kiungo Nizar Khalfan aliyekuwa anacheza Marekani na mshambuliaji Said Bahanuzi 'Ortega' kutoka Mtibwa Sugar.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RASMI; DAMAYO AANGUKA MIAKA MIWILI JANGWANI JION HII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top