![]() |
Tenga leo |
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah
Tenga amesema kwamba katika sakata la beki wa kimataifa wa Tanzania, Kelvin
Patrick Yondan kudaiwa kusaini mara mbili, lazima kuna klabu moja imefanya uhuni,
maana yake anamtetea beki huyo kwamba hajasaini mara mbili.
Akijibu swali aliloulizwa kwenye Mkutano wake na Waandishi
wa Habari mchana wa leo, ofisi za TFF, Ilala mjini Dar es Salaam, Tenga alisema
kwamba kulingana na mfumo wa sasa wa usajili kupitia mtandao, shirikisho lake
halihusiki kabisa na usajili na kwamba hilo ni suala la mchezaji na klabu.
Tenga alisema anaamini klabu hizo zitamalizana zenyewe
kuhusu mchezaji huyo na akasema suala la Yondan kudaiwa kutoroshwa kambini,
Taifa Stars ili akasaini Yanga halina mantiki kwa sababu mchezaji huyo ni mtu mzima
ana akili zake timamu, ila kinachoendelea kwa sasa ni kelele za kinazi.
Wiki iliyopita, beki Yondan aliibuka anasaini Yanga, kabla
ya klabu yake, Simba aliyoichezea tangu mwaka 2006 kudai bado ina mkataba naye
na wapinzani wao hao wa jadi, wamefanya uhuni kuzungumza naye na kumsajili wakijua
hajamaliza mkataba na klabu yake.
Lakini Yondan mwenyewe alikana kusaini Simba na kusistiza
amesaini Yanga tu, waliompa Sh. Milioni 30 kwa mkataba wa miaka miwili.
0 comments:
Post a Comment