![]() |
Cameroon |
CAMEROON imekosa tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika
mwakani kwa mara ya pili mfululizo, baada ya visiwa vya Cape Verde kwa jumla ya mabao 3-2. Jana Camroon imeshinda
mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano dhidi ya Cape Verde mjini Yaunde.
Ikumbukwe Cape Verde iliilaza Cameroon 2-0 katika mechi yao kwanza,
hivyo wenyeji jana walitakiwa washinde si chini ya 3-0 ili kusonga mbele.
Cape Verde sasa imeweka historia kwa kufuzu mara ya kwanza
kwenye fainali hizo za kuwania kombe la Mataifa Afrika, zitakazofanyika mwakani
nchini Afrika Kusini.
Katika mechi nyingine ya kufuzu, Ethiopia ilivaana na Sudan
ambapo Ethiopia imeibuka na ushini wa mabao 2-0. Katika mechi ya kwanza Sudan
ilishinda 5-3. Ethiopia sasa imufuzu kupitia kwa sheria ya bao la ugenini baada
ya timu hizo kufungana jumla ya mabao 5-5.
Mechi kati ya Senegal na Ivory Coast ilivunjika juzi baada ya
mashabiki wa soka kuzua ghasia wakati wa mechi hiyo mjini Dakar.
Mashabiki hao wa Senegal, waliwasha moto na kuanza kurusha
mawe uwanjani wakati Ivory Coast, ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0, matokeo
ambayo yangeiondoa timu yao. Mashabiki wa Ivory Coast, walilazimika kuingia
uwanjani ili kukwepa ghasia hizo.
Wachezaji na mashabiki hao wa Ivory Coast walisindikizwa na Polisi
wa kupambana na ghasia ambao walirusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya
mashabiki wa Senegal.
Ripoti zinasema watu 10 akiwemo Waziri wa Michezo wa Senegal,
Hadhi Malick Gakou, walijeruhiwa kwenye vurugu hizo zilizotokea katika Uwanja
wa Leopold Sedar Senghor.
Ghasia hizo zilianza wakati mshambuliaji nyota wa Ivory
Coast, Didier Drogba, alipofunga bao lake la pili kwa mkwaju wa penalti, huku zikiwa
zimesalia dakika 15 mechi hiyo kumalizika.
Kama mechi hiyo ingelimalizika matokeo yakiwa hivyo, Ivory
Coast ingeliibuka na ushindi wa jumla wa mabao 6-2 na kusonga mbele.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) halijatoa taarifa yoyote
kuhusiana na tukio hilo, lakini maafisa wa Shirikisho la Soka Senegal,
wamesema, timu hiyo ya Senegal huenda ikaadhibiwa vikali na CAF.
MATOKEO KAMILI NA TIMU ZILIZOFUZU:
Ethiopia 2-0 Sudan - Addis Ababa
Matokeo ya Jumla: Sudan 5-5 Ethiopia
Ethiopia wamefuzu kwa faida ya mabao ya ugenini
Cameroon 2-1 Cape Verde
-Yaounde-
Matokeo ya Jumla: Cape Verde 3-2 Cameroon
Cape Verde wamefuzu kwa mara ya kwanza fainali zijazo za
Afcon 2013 kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2.
Angola 2-0 Zimbabwe – Luanda
Matokeo ya Jumla: Angola 3-3 Zimbabwe
Angola wamefuzu kwa faida ya mabao ya ugenini.
MECHI ZA JUMAMOSI (Oktoba 13, 2014)
Malawi 0-1 Ghana - Lilongwe
Matokeo ya Jumla: Ghana 3-0 Malawi
Ghana imefuzu kwa mara nyingine
Botswana 1-4 Mali - Gaborone
Matokeo ya Jumla: Mali 7-1 Botswana
Mali imefuzu
Uganda 1-0 Zambia - Kampala
Matokeo ya Jumla: Uganda 1-1 Zambia
Zambia wameshinda kwa penalti 9-8 na kufuzu
Nigeria 6-1 Liberia - Calabar
Matokeo ya Jumla: Nigeria 8-3 Liberia
Nigeria imefuzu
Tunisia 0-0 Sierra Leone - Monastir
Matokeo ya Jumla: Sierra Leone 2-2 Tunisia
Tunisia wamefuzu kwa faida ya mabao ya ugenini
Senegal 0-2 Ivory Coast - Dakar
Mechi imevunjwa kwa sababu ya vurugu za mashabiki
Matokeo: Morocco 4-0 Msumbiji - Marrakech
Matokeo ya Jumla: Msumbiji 2-4 Morocco
Morocco imefuzu