Msanii Edson Wilson, aka Baby Boy, (pichani) ambaye yupo chini ya lebo ya Zizzou Entertainment, ametoa wimbo mpya
uitwao Hey ambao tayari
umekwishafanyiwa video na kampuni ya Inzy Entertainment, ambayo amesema hiyo ni
zawadi kwa mashabiki wake baada ya kimya cha muda mrefu na amewaambia wakae
mkao wa kula kwa vigongo zaidi.