• HABARI MPYA

    Sunday, October 14, 2012

    MABAO YA DROGBA YALIVYOCHAFUA AMANI SENEGAL, DAKAR YANUKA MOSHI

    Kimenuka... Drogba akilindwa na Polisi wakati akitolewa uwanjani.
    Shabiki wa Senegal akidakwa na polisi baada ya kuingia uwanjani wakati Didier Drogba (kulia) akitaka kupiga penati iliyowapa Ivory Coast uongozi wa mabao 2-0 dhidi ya Senegal katika mechi yao ya kuwania kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2013) kwenye Uwanja wa Leopold Sedar Senghor mjini Dakar, Senegal jana, Octoba 13, 2012. (Picha: AP)
    Hatari...!  Mashabiki wa 'chama' la kina Drogba wakihaha kujiokoa jana baada ya vurugu kuibuka katika mechi yao dhidi ya Senegal.

    Duh...! Kimenuka hadi kitaa.... mashabiki wa Senegal wakikimbia mitaani huku wakiandamwa na mabomu ya machozi baada ya kuzuka kwa vurugu uwanjani jana.

    Yaya Toure (kulia) na wachezaji wenzake wa Ivory Coast wakitolewa uwanjani na 'FFU' wa Senegal baada ya vurugu zilizotokea uwanjani jana.


    Sasa uwanjani hapakaliki tena...!

    Ni vurugu mtindo mmoja baada ya mashabiki wa Senegal kukasirishwa na kipigo cha Ivory Coast dhidi ya timu yao jana.

    Wachezaji Ivory Coast wakitolewa uwanjani.

    Wachezaji wakitolewa uwanjani wakisindikizwa na polisi baada ya mawe, chupa na vitu mbalimbali  kurushwa uwanjani na mashabiki wenye hasira wa Senegal waliokasirishwa kuona timu yao ikichapwa na kina Drogba.

    Mashabiki wa Ivory Coast wakihaha kujiweka pamoja ili kujiokoa jana.



    Kimenuka mwanaa... hapakaliki tena uwanjani!


    DAKAR, Senegal 
    Mechi muhimu ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Senegal na Ivory Coast imefutwa baada ya mashabiki kuvamia uwanja mjini Dakar juzi.

    Mashabiki wa wenyeji walianza kwa kuwasha moto majukwaani na kurusha mawe na vitu vingine uwanjani wakati Senegal wakiwa nyuma kwa mabao 2-0, matokeo ambayo yangewatoa katika michuano hiyo.

    Mashabiki wa Ivory Coast walikimbilia uwanjani kuepuka mashambulizi.

    Mashabiki na wachezaji wa Ivory Coast baadaye walitolewa nje na polisi, ambao walifyatua mabomu ya machozi kuelekea kwenye majukwaa yaliyofurika mashabiki.

    Taarifa zimesema kuwa takriban wati 10 -- akiwamo Waziri wa Michezo wa Senegal,Hadji Malick Gakou -- walijeruhiwa katika vurugu hizo kwenye Uwanja wa  Leopold Sedar Senghor.

    Vurugu hizo zilitokea baada ya mshambuliaji wa Ivory Coast, Didier Drogba kufunga goli lake la pili kwa njia ya penati, huku zikiwa zimebaki dakika 15 kabla mechi kumalizika. Kabla ya goli hilo la penati lililokuwa la 58 kwake kuifungia Ivory Coast, Drogba alifunga goli la kwanza katika mechi hiyo kwa njia ya 'fri-kiki'. 

    Matokeo hayo yangeiwezesha Ivory Coast kuongoza kwa jumla ya mabao 6-2 baada ya kushinda pia kwa mabao 4-2 katika mechi yao ya kwanza.

    "Vyakula, vinywaji na chochote kile kilichoweza kurushwa kilirushwa uwanjani, kutoka katika kona tofauti," Chris Fuglestad, mwanafunzi wa Marekani anayesoma mjini Dakar, aliiambia BBC.

    Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) bado halijatoa taarifa rasmi kuhusiana na tukiuo hilo. Lakini afisa mmoja wa Senegal alikaririwa akisema kwamba sasa timu yao itafungiwa na Caf.

    Wachezaji ndugu wa Manchester City, Yaya na Kolo Toure walikuwamo katika kikosi cha Ivory Coast, na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England ilisema katika taarifa yake kuwa: "Yaya na Kolo Toure wote wako salama baada ya vurugu za mashabiki kuvunja mechi wakati Senegal walipoikaribisha Ivory Coast mjini Dakar."

    SOURCE: straikamkali.blogspot.com
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MABAO YA DROGBA YALIVYOCHAFUA AMANI SENEGAL, DAKAR YANUKA MOSHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top