• HABARI MPYA

    Tuesday, November 20, 2012

    CHAGUZI ZA TFF...


    Na Prince Akbar
    MCHAKATO wa uchaguzi wa Chama cha Soka Katavi (KAREFA), umefutwa kutokana na wagombea watano kati ya nane vyeti vyao vya elimu ya sekondari kuwa na utata. Mchakato wa uchaguzi huo utaanza upya Novemba 21 mwaka huu.
    Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, mchakato wa uchaguzi wa Chama cha Wataalamu wa Tiba ya Michezo Tanzania (TASMA) utaanza upya Novemba 26 mwaka huu baada ya mchakto wa sasa kupata wagombea kwenye nafasi mbili tu za Kamati ya Utendaji ya chama hicho.
    Mchakato wa uchaguzi wa RUREFA utaanza Novemba 26 mwaka huu na Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA itapewa maelekezo ya usimamiaji wa uchaguzi huo baada ya mchakato wa awali kuwa umefutwa kutokana na kufanyika bila kuzingatia kanuni za uchaguzi.
    Wakati huo huo TFF, itakuwa na mkutano na Waandishi wa Habari utakaofanyika keshokutwa, saa 6:00 mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa shirikisho hilo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: CHAGUZI ZA TFF... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top