Kocha wa
Sudan, Mubarak Suleiman akifuatilia mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya
Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Uwanja wa Mandela, Namboole,
Kampala, Uganda kati ya timu yake na Somalia, uliomalizika kwa sare ya bila
kufungana. Kocha huyo anatumikia adhabu kwa kosa la kutohudhuria Mkutano na Waandishi
wa Habari, baada ya kufungwa mabao 2-0 na Tanzania Bara Jumapili.