Nafasi ya mshambuliaji Mghaha, Daniel Akuffo (pichani) katika klabu ya Simba itazibwa na kiungo Mganda, Mussa Mudde. Akuffo alisajiliwa Simba mwanzoni mwa msimu baada ya kutemwa kwa Mudde, aliyekuwa majeruhi. Lakini kutokana na Mghana huyo kushindwa kung'ara Msimbazi, sasa Mudde aliyepona anarejeshwa kikosini Simba. Tayari Simbe imekwishatangaza beki Mkenya Paschal Ochieng atatemwa na nafasi yake anachukua beki Mganda, Joseph Owino kutoka Azam FC. |