• HABARI MPYA

    Tuesday, November 20, 2012

    HIVI NDIVYO SIMBA NA AZAM WALIVYOFANYA BIASHARA YA OWINO


    Joseph Owino anarudi nyumbani Msimbazi
    Na Mahmoud Zubeiry
    AZAM FC wanataka Sh. Milioni 10 pamoja na kiungo Uhuru Suleiman kutoka Simba, ili wawape beki Mganda Joseph Owino.
    Habari za ndani, ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka Azam, zinasema kwamba tayari makubaliano yamefikiwa lakini, Simba inaonekana kusuasua kutekeleza makubaliano hayo.
    Azam wanadai wamekubaliana na Simba walipe fedha hizo Sh Milioni 10 na kumuidhinisha Uhuru kuhamia Chamazi, lakini suala la fedha bado halijatekelezwa.
    “Tena hapo bado kuna kesi ya fedha nyingine, Sh. Milioni 5, ambazo Simba wanadaiwa na Uhuru, sisi tumekubali kumpa fedha hizo Uhuru, halafu wao tutawakata kwenye mapato ya mlangoni katika mechi yetu na wao ya marudiano,”kilisema chanzo kutoka Azam.
    Lakini upande wa Simba nao wanasema fedha zote, Sh Milioni 15 walikubaliana zikatwe katika mapato ya milangoni.
    Simba imeamua kumrejesha Owino, ili kuimarisha safu yake ya ulinzi, ambayo imeonekana kuyumba katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Lakini pia hiyo ni nafuu kwa beki huyo Mganda, ambaye ameshindwa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha Azam chini ya makocha wote, kuanzia Mserbia Boris Bunjak aliyefukuzwa na huyu wa sasa Muingereza, Stewart Hall aliyerejeshwa kazini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: HIVI NDIVYO SIMBA NA AZAM WALIVYOFANYA BIASHARA YA OWINO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top