• HABARI MPYA

    Tuesday, November 20, 2012

    SERENGETI BOYS WAINGIZA MILIONI 23 TU

    Farid Mussa Shah wa Serengeto kulia akichuana na beki wa Kongo Brazzaville Tmouele Ngampio katika mechi hiyo

    Na Princess Asia
    MECHI ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Tanzania, Serengeti Boys na Kongo Brazzaville iliyochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza Sh. 23,021,000.
    Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, mapato hayo yametokana na washabiki 18,022 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 10,000, sh. 5,000, sh. 2,000 na sh. 1,000. Washabiki 15,850 walikata tiketi za sh. 1,000.
    Amesema asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 3,511,677.97 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 5,956,635), usafi na ulinzi (sh. 2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000), umeme (sh. 300,000) na ulinzi wa mechi (sh. 3,500,000).
    Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 1,000,537, asilimia 10 ya uwanja sh. 500,269, asilimia 5 ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) sh. 250,134, asilimia 45 ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,251,209, asilimia 20 ya TFF (sh. 1,000,537) na Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) sh. 50,027.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SERENGETI BOYS WAINGIZA MILIONI 23 TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top