Winga wa Yanga mwenye kasi na chenga za maudhi, Mrisho Khalfan Ngassa aliondoka jana kwenda Uingereza kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya West Ham United ya huko. Ngassa, mtoto wa kiungo wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Simba ya Dar es Salaam, aliondoka na wakala wake Yussuf Bakhresa kwenda kujaribu bahati yake. bongostaz inamtakia kila la heri mchezaji huyo.
0 comments:
Post a Comment