BENDI ya muziki wa dansi ya Mashujaa Musica, imezidi
kuibomoa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ baada ya kumnyakua mnenguaji wake mahiri, Lillian Tungaraza
maarufu kama ‘Lilli Internet’.
Aidha, Mashujaa pia imemuongeza katika safu yake mpapasa
gitaa la solo ambaye alipata kuzitumikia bendi kadhaa ikiwemo Twanga, Pepeta,
Ally Akida
Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Meneja wa Mashujaa
Band Maximilian Luhanga alisema kwamba wameamua kuwachukua wanamuziki hao ili
kuimarisha bendi yao katika idara hizo.
Alisema pamoja na kuimarisha idara hizo pia, wanaamini
uzoefu na umahiri walionao wasanii hao utasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza
kiwango cha bendi yao ambayo kwa sasa imeingia rasmi katika ushindanmi wa
kimuziki.
Aliongeza kuwa tayari wasanii hao wameshasaini mikataba ya
kuitumikia bendi hiyo kwa miaka miwili na Jumatano watapanda kwenye jukwaa la
bendi hiyo kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa Nyumbani Lounge.
Hii ni mara ya pili kwa Mashujaa kuibomoa Twanga Pepeta,
kwani mapema mwaka huu ilimnyakua Charles Gabriel ‘Chaz Baba’.
0 comments:
Post a Comment