• HABARI MPYA

    Thursday, March 01, 2012

    PATO SASA SPANA MKONONI, AUMIA TENA AC MILAN, KUWAKOSA ARSENAL NEXT WEEK

    MSHAMBULIAJI wa AC Milan, Alexandre Pato amerejea tena kwenye chumba cha wagonjwa, baada ya kuumia misuli, vinara hao wa Ligi Kuu ya Italia, Serie A wamesema leo.
    Kuumia huko ni kwa mara ya 13 kwa Mbrazil huyo ndani ya miaka miwili na sasa anatarajiwa kukaa tena nje ya Uwanja kwa wiki kadhaa, maana yake ataikosa mechi ya Ligi ya Mabingwa  ya marudiano hatua ya 16 Bora dhidi ya Arsenal mjini London, Machi 6.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amechezea mechi 17 tu The Rossonieri msimu huu na kufunga mabao manne.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PATO SASA SPANA MKONONI, AUMIA TENA AC MILAN, KUWAKOSA ARSENAL NEXT WEEK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top