Tetesi za J'pili magazeti ya Ulaya

VAN PERSIE AENDA TIMU YA ETO'O

WAMWAGA 'hela chafu', klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi wako tayari kumpa ofa Nahodha wa Arsenal, mshambuliaji Robin van Persie mwenye umri wa miaka 28, ya mshahara wa pauni 300,000 kwa wiki.
KLABU ya Chelsea imejiweka katika nafasi ya kuzipiga bao Manchester City na United katika mbio za kuwania saini ya kiungo wa Lille, mwenye umri wa miaka 21, Eden Hazard - hata kabla hawajatwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya jana.
KLABU ya Real Madrid inaandaa dau la pauni Milioni 50 kwa ajili ya kumnasa shujaa wa ubingwa wa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya England, Manchester City, Sergio Aguero, mwenye umri wa miaka 23.
KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho anataka kuibomoa timu yake ya zamani, Chelsea kwa kumchukua mchezaji wao, Ramires mwenye umri wa miaka 25 ahamishie makali yake Bernabeu.
Sergio Aguero
Aguero joined Manchester City from Real Madrid's city rivals Atletico in August
KOCHA Sir Alex Ferguson ametoa ofa ya pauni Milioni 4 kwa mchezaji wa Crewe na timu ya taifa ya England chini ya umri wa 18, Nick Powell ili akakomazwe zaidi kisoka Manchester United.
WASHAMBULIAJI Marouane Chamakh mwenye umri wa miaka 28, na Nicklas Bendtner mwenye miaka 24, ni wawili kati ya wachezaji 10 ambao wanaweza kuondoka Arsenal wakati Arsene Wenger akiunda upya kikosi chake.
KLABU ya Manchester United ilikuwa imetenga dau la pauni Milioni 9.7 kumnasa kiungo wa Udinese, mwanasoka wa kimataifa wa Ghana, Kwadwo Asamoah mwenye umri wa miaka 23, lakini klabu yake imekataa.
KLABU ya Real Madrid inawataka viungo Luka Modric mwenye umri wa miaka 26, na Ramires mwenye miaka 25, kutoka Tottenham na Chelsea .

SUAREZ KWAHERI LIVERPOOL

KLABU ya Liverpool iko kwenye hatari ya kuwapoteza nyota wake Luis Suarez na Martin Skrtel kutokana na wamiliki wa klabu hiyo, Wamarekani kutaka kupunguza gharama za uendeshaji timu.
KOCHA wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas anaweza kupewa nafasi ya kazi ya kurithi mikoba ya Kenny Dalglish aliyefukujzwa Liverpool.
KLABU ya Chelsea inaweza kuwa tayari kumtwaa Redknapp awe bosi wa Stamford Bridge.
KOCHA wa zamani wa England, Fabio Capello amejitoa kwenye mbio za kuwania kazi Chelsea.
Steve Kean
Kean's Blackburn were relegated from the Premier League this season
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney alipata ajali katika wiki za mwishoni mwa msimu na maofisa wa England wamesema atanufaika na mapumziko ya wiki mbili kupona kabisa maumivu yake na uchovu wowote.
KOCHA Steve Kean hataondolewa katika klabu ya Blackburn, lakini atahamishiwa kwenye majukumu mengine na kuendelea kupata mshahara ule ule anaopata sasa.
KOCHA anayewaniwa na Aston Villa, Ole Gunnar Solskjaer ameiambia klabu yake ya sasa, Molde kwamba anataka kuhamia Ligi Kuu ya England.
KLABU ya West Brom inajiandaa kumchukua kocha wa Birmingham, Chris Hughton wiki hii akiwa ndiye chaguo lao la kwanza kumrithi Roy Hodgson aliyechukuliwa timu ya taifa.

MANCHESTER CITY WAITESA UNITED...

HALMASHAURI ya Jiji la Manchester, imeamua kuchora bango lililoandikwa 'Blue Moon Way' - kusherehekea taji la kwanza la klabu ya Manchester City la Ligi Kuu ya England katika miaka 44.