• HABARI MPYA

    Friday, May 18, 2012

    BAYERN HAIJAFUNGWA NYUMBANI, CHELSEA WATAVUNJA MWIKO?


    Chelsea na kombe la FA
    Chelsea na kombe la FA

    Jupp Heynckes wa Bayern
    Jupp Heynckes-Bayern

    KLABU ya Bayern imeshinda mechi zake saba za nyumbani mfululizo kuelekea fainali hii dhidi ya Chelsea.
    Mara ya mwisho kwa pande hizi mbili kukutana, ilikua katika robo fainali ya mwaka 2005 ambapo Chelsea ilishinda 6-5 kwa jumla ya mabao ya ugenini na nyumbani.
    Wakati huo Petr Cech, John Terry, Ashley Cole, Frank Lampard na Didier Drogba wote walishiriki.
    Bayern inataraji kujiunga na Liverpool kama mojapo ya vilabu vitatu vilivyofanikiwa katika mashindano ya Kombe la Ulaya ikiwa watashinda kwa mara ya tano.
    Klabu iliyopata ushindi zaidi ya Bayern ni Real Madrid na AC Milan.
    Bayern imeshinda mara moja na kushindwa mara mbili mara tatu ilipochuana na upinzani kutoka kwa vilabu vya England.
    Hii ni mara ya sita katika Kombe la Ulaya kwa vilabu vya Ujerumani na England kupambana kwenye fainali -na ni mara moja tu ambapo vilabu kutoka Ligi ya Bundesliga kuibuka na ushindi.
    Ushindi wa Bayern utamfanya Jupp Heynckes kua kocha wa 19 kushinda kombe hili mara mbili, kufuatia ushindi wake wa 1998 alipokua akiifunza Real Madrid.
    Ikiwa uwanja wa nyumbani Bayern imeshinda mechi 13 kati ya 14 za michuano ya Ulaya, huku Chelsea ikiwa imeshinda mara moja tu ikiwa safarini katika michuano ya msimu huu.
    Mara pekee ambapo Chelsea ilifikia fainali ilikua mwaka 2008 mjini Moscow iliposhindwa na Manchester United kupitia mikwaju ya penalti.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BAYERN HAIJAFUNGWA NYUMBANI, CHELSEA WATAVUNJA MWIKO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top