Tetesi za J'nne magazeti ya Ulaya

LIVERPOOL WAMVAMIA MCHEAZAJI WA ARSENAL

KLABU ya Arsenal ikiwa katika harakati za kumsajili mshambuliaji wa Fulham, Clint Dempsey, inagundua Liverpool nayo inamtaka mchezaji huyo.
MCHEZAJI anayewaniwa na Tottenham, Loic Remy, mshambuliaji wa Marseille ya Ufaransa mwenye umri wa miaka 25, amesema anataka kwenye klabu hiyo ingawa ana wasiwasi hali ya kifedha itamfanya auzwe.
KLABU ya Tottenham Hotspur inataka kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa kumsajili beki hodari wa Ajax Amsterdam ya Uholanzi, Jan Vertonghen.
KLABU ya Manchester United imetupa ndoana zake kwa beki la nguvu la Kiholanzi, Jan Vertonghen, ambalo pia linawaniwa na Tottenham'.
KIUNGO wa Porto mwenye umri wa miaka 25, ambaye ana thamani ya pauni Milioni 25, Joao Moutinho, ambaye amekuwa akichunguzwa na klabu ya Chelsea, amesema kwamba atachangamkia ofa ya kwenda kucheza England
Kama watabaki katika Ligi Kuu ya England, klabu ya QPR imepanga kumsajili kwa dau la pauni Milioni 7, winga  wa Wigan, Victor Moses.
KINDA mwenye umri wa miaka 17, mshambuliaji wa klabu ya Libertad ya Peru, anayewaniwa na Chelsea ya England, imebainika anawaniwa pia na vigogo wa Hispania, Barcelona na Real Madrid.
KINDA  mwenye umri wa miaka 17, anayepewa thamani ya juu, mshambuliaji wa Peru, Andy Polo, aliyefikiwa angekwenda Arsenal, ameamua kutua Genoa ya Italia kwa dau la pauni Milioni 4.

GUARDIOLA AKATAA BONGE LA OFA CHELSEA



ALIYEKUWA kocha wa Barcelona, Pep Guardiola kwa mara ya pili amechomoa ofa ya kujiunga na Chelsea ya England, ingawa alikuwa anapewa mkwanja mnene, wa pauni Milioni 12 kwa mwaka.
BEKI wa Aston Villa, Carlos Cuellar ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba ataondoka katika klabu hiyo.

PAMBA MPYA ARSENAL...

KLABU ya Arsenal imezindua jezi zake mpya katika video, inayomuonyesha mshambuliaji wake nyota, Robin van Persie, na kipa Wojciech Szczesny akienda kutoa mpira kwenye roof la gari la kocha wao, Arsene Wenger.