Published: Today at 15:43
MARK HUGHES amesema kwamba hataitumia mechi
kati ya timu yake, QPR dhidi ya Manchester City kwa vita zake binafsi.
Rangers wanahitaji pointi moja tu, kuzima
ndoto za Manchester City kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Jumapili, iwapo Manchester
United wataifunga Sunderland- nao kujihakikishia kubaki Ligi Kuu.
Lakini mechi hiyo itakayopigwa Etihad imekuwa
gumzo kubwa, baada ya Hughes kufukuzwa ‘kinyama’ na City mwaka 2009 na nafasi
yake kuchukuliwa na Roberto Mancini.
Hughes, pamoja na hayo amekataa kuitumia
mechi hiyo kama sehemu ya kulipa kisasi.
Alisema: “Watu wamekuwa wakisema maneno hayo,
lakini siyo mawazo yangu kabisa.
“Pointi yangu ni kuangalia kikamilifu juu
ya kipi tunatakiwa kufanya, kama ambavyo ungetarajia.
“Tunakabiliwa na mchezo mkubwa na mgumu. Haitakuwa
rahisi kwa Manchester City kama timu imara.


.png)
0 comments:
Post a Comment