• HABARI MPYA

    Friday, May 18, 2012

    MDHAMINI TUZO ZA TASWA KUJULIKANA JUMAPILI


    Wadau wa soka, Abeid Mziba juu kulia, Ibrahim Masoud na Juma Mgunda. Soka husisimua katika tuzo za TASWA.

    CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) Jumapili Mei 20, 2012 saa nne asubuhi kitatangaza mdhamini wa Tuzo za Mwanamichezo Bora wa Tanzania kwa mwaka 2011.
    Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando ameiambia BIN ZUBEIRY  mchana huu kwamba, mdhamini huyo atatangazwa kwenye mkutano ambao ataufanya Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto pamoja na mdhamini wa tuzo hizo, ambapo mkutano huo utafanyika kwenye mgahawa mpya uitwao City Sports  &  Lounge uliopo jirani na mnara wa askari makutano ya barabara ya Samora na Azikiwe, Posta Dar es Salaam.
    Amesema TASWA inachukua fursa hii kuwaalika waandishi wote wa habari za michezo kuhudhuria kwenye mkutano huo ili tuweze kuanza pamoja katika mbio hizi za kuelekea kwenye Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Mwaka 2011.
    Tayari TASWA imekwishatangaza Kamati ya Tuzo, hivyo baada ya mkutano huo taratibu nyingine zitatangazwa kwa kadri zitakavyokuwa zimekamilishwa na Kamati Maalum ya Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Tanzania.
    Kwa miaka mitano iliyopita walioshinda Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa TASWA walikuwa ni  Samson Ramadhani (2006),  Martin Sulle  (2007),  Mary Naali (2008), ambao wote ni wanariadha, wakati 2009 na 2010 alikuwa mcheza netiboli Mwanaidi Hassan.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MDHAMINI TUZO ZA TASWA KUJULIKANA JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top