• HABARI MPYA

    Friday, May 18, 2012

    NDUGU YAKE VAN PERSIE AOMBA KUFUNDISHA YANGA


    Robin van Persie

    JUMLA ya makocha 24 kutoka nchi mbalimbali, wamejitokeza kuomba kazi ya kufundisha klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, nafasi iliyoachwa wazi na Mserbia Kostadin Bozidar Papic.
    Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu amaeiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba, makocha waliojitokeza ni kutoka Uholanzi, anakotoka mshambuliaji wa Arsenal Robin van Persie, Scotland anakotoka kocha wa Manchester United, Alex Ferguson, Serbia anakotoka beki wa Man United Nemanja Vidic na Ujerumani anakotoka Mesut Ozil mshambuliaji  wa Real Madrid.
    Sendeu alisema wengine wanatokea England anakotokea Wayne Rooney, Brazil anakotokea Neymar na Ureno anakotokea Cristiano Ronaldo.
    Sendeu alisema Kamati ya Ufundi bado inapitia wasifu wa makocha hao kabla ya kupendekeza watatu wa kuingia kwenye mchujo wa mwisho, ambao miongoni mwao atapatikana kocha mpya wa Yanga.
    Aidha, Sendeu alisema kwamba Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Yanga, imeahairisha Mkutano wake na Wazee, ili kushughulikia mambo mengine yaliyojitokeza ikiwa ni pamoja na mapendekezo ya Yussuf Manji.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NDUGU YAKE VAN PERSIE AOMBA KUFUNDISHA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top