LEO haikuwa siku nzuri kwa Azam kwa ujumla. Wakati Azam A ikiukosakosa ubingwa wa Kombe la Urafiki, kwa kufungwa na Simba SC, Dar es Salam, timu ya soka ya vijana ya Azam
FC, Azam Academy leo imefungwa 1-0 kwenye michuano ya Rollingston inayoendelea
nchini Burundi, katika mechi ambayo mgeni rasmi alikuwa rais wa Burundi, Perre
Nkurunziza.
Hata hivyo, kipigo hicho
hakiiathiri Azam, kwani tayari imekwishafuzu Robo Fainali, baada ya kushinda
mechi zake mbili za awali 1-0 dhidi ya Kyazanga FC ya Uganda na 3-0 dhidi ya
Nyirakongo Academy ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Azam sasa itamenyana na Mjini
Magharibi katika Robo Fainali ya michuano hiyo, Jumanne.
0 comments:
Post a Comment