![]() |
Thomas Ulimwengu wa Ngorongoro |
Na Princess Asia
TIMU ya taifa ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 20,
Ngorongoro Heroes, leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Chamazi, kumenyana na
vijana wenzao wa Rwanda katika mchezo wa kirafiki, kujiandaa na mechi dhidi ya
Nigeria Julai 29, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika.
Rwanda ‘Nyigu Wadogo’, waliwawasili Dar es Salaam jana
mchana Dar es Salaam kwa ndege ya shirika la ndege la Rwanda kwa ajili ya mechi
mbili za kirafiki dhidi ya Ngorongoro Heroes.
Rwanda yenye msafara wa watu 27 wakiwemo wachezaji 20, imefikia
katika hoteli ya Sapphire na baada ya mechi ya leo, timu hizo zitacheza tena
keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ngorongoro Heroes iko kambini chini ya Kocha wake, Mdenmark Jakob
Michelsen na msaidizi wake Mohamed Adolf Rishard.
Mechi dhidi ya Nigeria ambayo ni ya kwanza ya raundi ya pili
kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini
Algeria itachezwa Julai 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment