Tetesi za J'mosi magazeti ya Ulaya


WEST HAM YAMNASA MAIGA

KLABU ya West Ham ipo karibu kumsaini kwa dau la pauni Milioni 5, mshambuliaji mwenye umri wa miaka 24 wa Sochaux ya Ufaransa, Modibo Maiga, ambaye alikaribia kujiunga na Newcastle Januari mwaka huu, kabla dili halijafa kutokana na matatizo yake ya goti.
Sochaux's Modibo Maiga
Maiga ni mwanasoka wa kimataifa wa Mali na alicheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2010
MABINGWA wa Ureno, Porto wameziaimbia klabu za Manchester United na Tottenham timu itakayotoa pauni Milioni 30, ndio itapata saini ya kiungo wao, oao Moutinho, mwenye umri wa miaka 25.
KLABU ya Manchester United inajiandaa kukata dau la pauni Milioni 10 kumnasa beki Leighton Baines, mwenye umri wa miaka 27, kutoka Everton.
KLABU za Blackburn na Wolves zimejiunga kwenye mbio za kuwania saini ya mshambuliaji mwenye thamani ya pauni Milioni 2.5 wa Leeds, Ross McCormack, mwenye umri wa miaka 25, katika harakati za kujiimarisha kwa mapambano ya kurejea Ligi Kuu.
KLABU ya Birmingham imeanza mazungumzo na Arsenal juu ya uhamisho wa mkopo wa kinda wa timu ya taifa ya vijana ya England chini ya umri wa miaka 19, mshambuliaji Benik Afobe.
KOCHA wa Norwich, Chris Hughton anataka kurejea klabu yake ya zamani, Birmingham si kwa ajili ya kazi, bali kumuiba beki Curtis Davies, mwenye umri wa miaka 27.

HATIMA YA JT SASA MIKONONI MWA FA 

MABEKI John Terry wa Chelsea, mwenye umri wa miaka 31, na Anton Ferdinand wa QPR, mwenye umri wa miaka 27, kesi yao sasa itahamia Chama cha Soka (FA), baada ya mhakama kumsafisha JT kwamba hana hatia.  Anton analalamika kutolewa kashfa za kibaguzi sambamba na maneno ya ngono na Terry.
KLABU ya Chelsea imepata pauni Milioni 47.3 kwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mei mwaka huu, kikiwa ni kiasi cha zaidi ya pauni Milioni 20 dhidi ya Manchester United, ambao walishindwa hatua ya 16 bora.
Sunderland's Lee Cattermole
Cattermole amecheza mechi 73 Sunderland tangu ajiunge nao kutoka Wigan Agosti 2009
MUSTAKABALI wa Jody Craddock katika klabu ya Wolves uko shakani, baada ya mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36 kutemwa kwenye ziara ya kujia ndaa na msimu mpya nchini Ireland.
KOCHA wa Sunderland, Martin O'Neill inataka kumtia pingu Lee Cattermole, mwenye umri wa miaka 24, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao, kwa kumsainihsa mkataba mpya  Stadium of Light.
Michael Laudrup amesema kwamba Swansea watatakiwa kusubiri hadi baada ya Michezo ya Olimpiki kabla ya kumtia pingu Scott Sinclair, mwenye umri wa miaka 23, kwa kumsainisha mkataba mpya.
WAKALA wa Alberto Aquilani, amesema kwamba, kiungo huyo Mtaliano wa Liverpool mwenye umri wa miaka 28, atabakia Anfield msimu ujao.