• HABARI MPYA

    Saturday, July 14, 2012

    NI MORO NA MWANZA FAINALI COPA COCA COLA 2012


    Na Princess Asia
    MOROGORO na Mwanza ndizo zitakazomenyana katika fainali ya Copa Coca Cola kesho Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
    Morogoro ilikata tiketi ya kuingia fainali katika mchezo wa jioni jana, baada ya kuifunga Tanga mabao 3-1, Uwanja wa Karume.
    Mwanza yenyewe ilijipatia tiketi ya kucheza fainali ya michuano hiyo, baada ya kuilaza Temeke mabao 3-1 katika mchezo wa asubuhi, uliofanyika Uwanja wa Karume pia.
    Hadi dakika 90 za kawaida zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1. Mwanza walitangulia kufunga dakika ya tatu kupitia kwa Jamal Mtegeta kabla ya Temeke kusawazisha kwa penalti dakika ya 56 iliyowekwa wavuni na Baraka Ntalukundo.
    Mabao mengine ya Mwanza yaliyoipatia tiketi ya kucheza fainali keshokutwa (Jumapili) yalifunga katika dakika 30 za nyongeza. Mtegeta alitikisa wazu dakika ya 94 kabla ya Dickson Ambundo kukwamisha la tatu dakika ya 108.
    Nusu fainali ya pili itachezwa leo jioni ikikutanisha timu za Morogoro ambayo kwenye robo fainali iliibamiza Mara mabao 4-0 na Tanga iliyopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI MORO NA MWANZA FAINALI COPA COCA COLA 2012 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top