![]() |
Saintfiet kushoto na BIN ZUBEIRY |
KAMA ulikuwa hujui, Kocha Mkuu wa Yanga, Tom Saintifiet 'Mtakatifu Tom' amefungwa vyuma katika magoti yake yote mawili kwa vile aliumia kipindi alipokuwa akicheza mpira na ndiyo sababu ya kustaafu soka mapema.
Saintfiet, ambaye ni raia wa Ubelgiji aliichezea klabu ya Boom FC ya nchini humo kabla ya kutundika daruga akiwa na umri wa miaka 24 na kujikita rasmi katika kufundisha akiwa kocha kijana kabisa Ubelgiji.
Akizungumza na Mwanaspoti, Saintfiet aliyekuwa akicheza nafasi ya kiungo alisema: "Napenda kucheza, lakini hata hivyo daktari wangu alinishauri nisicheze kwa sababu miguu yangu ina matatizo, hivi unavyoiona nina vyuma ndani."
Wakati anaeleza hayo, Saintfiet alikuwa akionyesha alama alizofanyiwa upasuaji.
Hata hivyo, Saintfiet aliyewahi kufundisha timu za taifa za Namibia, Zimbabwe na Ethiopia anapenda kucheza soka na amekuwa akihimiza watu wake wa benchi la ufundi wacheze mechi wenyewe kwa wenyewe na wakati mwingine anapogawa kikosi chake lazima wagawane timu na msaidizi wake, Fred Felix 'Minziro'.
SOURCE: Gazeti la Mwanaspoti
0 comments:
Post a Comment