![]() |
Mtakatifu Tom kulia, akiwa na kigogo wa Yanga, Seif Ahmad 'Magari' |
Na Mahmoud Zubeiry
KOCHA Mkuu
wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, Mbelgiji Tom Saintfiet ‘Mtakatifu Tom’,
amesema kwamba anatarajia mvua ya mabao katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, kutokana na uwezo mkubwa wa kufunga wa wachezaji wake, kuanzia
mabeki, viungo hadi washambuliaji.
Akizungumza
na BIN
ZUBEIRY jana, Mtakatifu Tom alisema kwamba mbali na washambuliaji
kufunga, pia mabeki wake na viungo wanafunga pia, na hilo linampa faraja sana.
Jana Yanga
ilicheza mechi ya mwisho ya kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu na
kushinda mabao 4-0 dhidi ya Moro united, Mrundi Didier Kavumbangu akifunga
mawili, mengine beki Juma Abdul na kiungo Shamte Ally.
“Kavumbangu
aliwahi kufunga pia tulipocheza na Sinza Stars, ninafurahia hilo, ni muhimu kwa
klabu kubwa, lakini pia wachezaji wengine wanaweza kufunga, Stefano Mwasyika,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul…tumecheza mechi 14 kabla ya ligi, zikiwemo
dhidi ya Sinza Stars na Kijitonyama Stars, tumefunga mabao 42 na tumefungwa
sita tu,”alisema Mtakatifu Tom.
Saintfiet alitaka
mechi moja dhidi ya timu inayocheza kama wapinzani wao wa kwanza katika Ligi
Kuu, Prisons na pia katika Uwanja mbaya kama ambao atachezea mechi ya kwanza ya
ligi hiyo, Sokoine mjini Mbeya na ndiyo maana timu hiyo ikacheza na Moro United
juzi kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kijitonyama.
Saintfiet
ameridhika na kiwango cha timu na sasa anasema timu iko tayari kwa Ligi Kuu,
akianza na Prisons iliyorejea Ligi Kuu msimu huu kwenye Uwanja wa Sokoine, Septemba
15.
Hiyo ilikuwa mechi ya 11, Saintfiet anashinda
Yanga katika mechi 12 tangu ajiunge nayo miezi miwili iliyopita, mbali ya ziwe
za mazoezini dhidi ya Sinza Stars na Kijitonyama Stars.
Ndani ya mechi hizo kuna mechi sita za
Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, ambalo
aliiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa tano wa michuano hiyo, ikipoteza mechi moja
tu ya kwanza dhidi ya Atletico ya Burundi, kwa kufungwa 2-0, mabao yote ya
Kavumbangu, ambaye baadaye ikamsajili.
REKODI YA SAINTFIET YANGA
1.
Yanga
Vs JKT Ruvu 2-0
2.
Yanga
Vs Atletico (Burundi) 0-2
3.
Yanga
Vs Waw Salam (Sudan Kusini) 7-1
4.
Yanga
Vs APR (Rwanda) 2-0
5.
Yanga
Vs Mafunzo (Z’bar) 1-1 (5-3penalti)
6.
Yanga
Vs APR (Rwanda) 1-0
7.
Yanga
Vs Azam 2-0
8.
Yanga
Vs African Lyon 4-0
9.
Yanga
Vs Rayon (Rwanda) 2-0
10. Yanga
Vs Polisi (Rwanda) 2-1
11. Yanga
Vs Coastal Union 2-1
12. Yanga
Vs Moro United 4-0
0 comments:
Post a Comment