• HABARI MPYA

    Friday, May 30, 2025

    MUKWALA MCHEZAJI BORA, FADLU KOCHA BORA LIGI KUU MWEZI MEI


    MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Uganda, Steven Dese Mukwala ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mwezi Mei – huku Kocha wake, Fadluraghman Davids raia wa Afrika Kusini akishinda Tuzo ya Kocha Bora mwezi huo.
    Mukwala aliye katika msimu wake wa kwanza Simba SC baada ya kuwasili kutoka Asante Kotoko ya Ghana amekuwa mshindi wa Tuzo hiyo dhidi ya mchezaji mwenzake, kiungo wa Ivory Coast, Jean Charles Ahoua na mshambuliaji wa Mashujaa FC ya Kigoma, Jaffat Salum Kibaya.
    Kwa upande wake Fadlu Davids ambaye amejiunga na Simba SC msimu huu akitokea Raja Casablanca ya Morocco alipokuwa Kocha Msaidizi – ameshinda Tuzo hiyo dhidi ya Mualgeria, Miloud Hamdi wa Yanga SC na Mmorocco Rachid Taoussi wa Azam FC. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MUKWALA MCHEZAJI BORA, FADLU KOCHA BORA LIGI KUU MWEZI MEI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top