• HABARI MPYA

    Tuesday, May 20, 2025

    MFUMO AMIS NA TAUSI KURAHISISHA KAZI ZA SANAA NCHINI


    NAIBU waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma @mwanafa amesema kuwa, Mfumo wa Artist Information Management System (AMIS) ambao umeunganishwa na TAUSI kutoka TAMISEMI umerahisisha usajili wa wasanii ambapo kati ya Julai 2024 hadi Aprili 2025 wasanii binafsi 844, vikundi 158, taasisi 39, kampuni 274 na kumbi za burudani 115 zimesajiliwa ili kukuza na kurahisisha sanaa nchini.
    Mhe. Mwinjuma ameeleza hayo Mei 20, 2025, Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mhe. Lucy Sabu Mbunge wa Viti Maalumu kuhusu mikakati ya serikali kuhakikisha sekta ya Sanaa na michezo inawanufaisha vijana kwa kuweka mifumo rasmi.
    Amesema, Serikali inaendelea kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa wasanii kupitia Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ambapo, kiasi cha shilingi Bilioni 5. 25 zimetolewa kupitia benki ya CRDB na NBC kote nchini.
    Vilevile, imeanzisha tozo ya hakimiliki kwa lengo la kuwanufaisha wabunifu wakiwemo wasanii ambapo kati ya Septemba 2023 hadi Aprili 2025, jumla ya shilingi Bilioni 1.55 zimekusanywa.
    Aidha, Mhe Mwinjuma ameeleza kuwa, ujenzi wa Akademia ya Michezo katika Chuo cha Maendeleo ya michezo Malya kwa lengo la kuibua vipaji hasa kwa vijana wenye umri mdogo ni miongoni mwa mikakati ya kuendeleza michezo. Pia mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA yanatumika kama njia ya kugundua na kukuza vipaji.
    Akijibu swali la nyongeza la Mhe. Lucy Sabu kuhusu kukamilika kwa Akademia hiyo, Mhe. Mwinjuma amesema kuwa ujenzi huo utakamilika mwezi Desemba 2025. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MFUMO AMIS NA TAUSI KURAHISISHA KAZI ZA SANAA NCHINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top