Shujaa wa Yanga leo ni kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Maxi Mpia Nzengeli aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 45 na mabingwa hao wa Tanzania Bara wamezawadiwa Sh. Milioni.
Pamoja na kufunga bao la ushindi, Nzengeli pia ameshinda Tuzo za Mfungaji Bora kwa mabao yake mawili jumla na Nyota wa Mchezo wa leo, wakati kiungo mwenzake wa Yanga, Mudathir Yahya Abbas ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano.
JKU, mabingwa wa Zanzibar ambao kwa kumaliza nafasi ya pili wamezawadiwa Sh. Milioni 30 — wametoa Kipa Bora wa mashindano, Ahmed Issa Haji na Mchezaji Bora Chipukizi, Nizar Abubakar anayecheza kwa mkopo kutoka Azam FC.
Jumla ya timu nane zimeshiriki michuano ya mwaka huu iliyoanzia hatua ya Robo Fainali, nyingine ni KMKM, Zimamoto na KVZ, zote za Zanzibar na Azam FC, Coastal Union na Singida Black Stars za Tanzania Bara.
Mabingwa wa msimu uliopita, Simba hawakushiriki michuano ya mwaka huu kwa sababu wanakabiliwa na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Simba SC ilitwaa taji la michuano hiyo iliyoanza mwaka jana kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC katika Fainali Uwanja wa New Amaan Complex, bao pekee la kiungo Msenegal, Babacar Sarr, dakika ya 77.
Sarr alifunga bao hilo akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na beki Israel Patrick Mwenda kufuatia mshambuliaji Mcameroon, Leandre Willy Essomba Onana kuangushwa nje kidogo ya boksi.
Msimu uliopita michuano hiyo ilishirikisha timu nne kuanzia hatua ya Nusu Fainali.
0 comments:
Post a Comment