TANZANIA imepewa pointi tatu na mabao matatu dhidi ya Kongo katika Kundi E kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026 kufuatia mchezo baina ya timu hizo kutofanyika Machi mwaka huu.
Mchezo huo haukufanyika kwa sababu Kongo ilikuwa inatumikia adhabu ya kufungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) — lakini baada ya kufutiwa adhabu leo, Taifa Stars imepewa ushindi.
Sasa Taifa Stars inafikisha pointi tisa na kusogea nafasi ya pili nyuma ya vinara, Morocco wenye pointi tano na mbele ya Zambia wenye pointi sita baada ya timu zote kucheza mechi tano kila moja.
Niger yenye pointi sita pia baada ya kucheza mechi nne ipo nafasi ya nne na Kongo ambayo haina pointi inashika mkia ikipoteza chee pointi 15 kutokana na adhabu.
Taifa Stars itakuwa na mechi mbili za kufuzu Kombe la Dunia mwezi Septemba dhidi ya Kongo ugenini na Niger nyumbani kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi E kwa kucheza na Zambia nyumbani mwezi Oktoba.
0 comments:
Post a Comment