• HABARI MPYA

    Friday, May 30, 2025

    NI AZAM FC MABINGWA WA LIGI YA VIJANA U20


    TIMU ya Azam FC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Fainali usiku wa jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Shujaa wa Azam FC jana alikuwa ni mshambuliaji Carlos Chasambi aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 11 akimalizia kwa kichwa krosi nzuri ya Ismail Ally kutoka upande wa kushoto wa Uwanja.
    Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, mabingwa wa msimu uliopita, Kagera Sugar walipoza machungu kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ken Gold hapo hapo Azam Complex.
    Mabao ya Kagera Sugar yalifungwa na Luquman Abubakar na Masanja Batano, wakati bao pekee la Ken Gold lilifungwa na Popah Richard.
    Ikumbukwe Azam FC ilifika Fainali baada ya kuwachapa Kagera Sugar 1-0, na Fountain Gate iliichapa Ken Gold 2-1 hapo hapo Azam Complex Jumanne.
    Safari ya Azam FC katika michuano hii hatua ya Nane Bora ilianzia Kundi A, ambako waliongoza kwa kuvuna ponti saba mbele ya Ken Gold iliyomaliza na pointi sita – hivyo kuzipiku Simba SC iliyomaliza na pointi mbili na Dodoma Jiji washindi wa pili wa msimu uliopita waliomaliza na pointi moja.
    Kwa upande wao Fountain Gate waliongoza Kundi B baada ya kuvuna pointi saba, ikiizidi tu wastani wa mabao Kagera Sugar, zote zikizipku Tanzania Prisons iliyomaliza na pointi tatu mna Yanga ambayo ilifungwa mechi zote tatu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI AZAM FC MABINGWA WA LIGI YA VIJANA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top