• HABARI MPYA

    Friday, May 16, 2025

    AL ITTIHAD YA BENZEMA YATWAA UBINGWA LIGI YA SAUDIA ARABIA


    TIMU ya Al Ittihad jana ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia ‘Saudi Pro League’ ikiwa na mechi mbili mkononi baada ya kutoka nyuma na kushinda mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Al Raed 3-1 Uwanja wa King Abdullah Sport City Jijini Buraidah.
    Kwa ushindi huo, Al Ittihad iliyo chini ya Kocha Mfaransa, Laurent Blanc inaifikisha pointi 77 katika mchezo wa 32, tisa zaidi ya Al Hilal wanaofuatia na hilo linakuwa taji la 10 la Ligi kwao kihistoria na la kwanza tangu mwaka  2023.
    Haukuwa ushindi mwepesi, kwani wenyeji walitangulia na bao la beki Mcameroon, Omar Gonzalez dakika ya tisa, huku Nahodha wake, gwiji wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria, Karim Benzema ambaye ni majeruhi akishuhudia mchezo pembeni ya Uwanja.
    Hata hivyo, Al Ittihad ilizunduka kwa mabao ya mshambuliaji Mholanzi, Steven Bergwijn dakika ya 21, kiungo Mreno Danilo Pereira dakika ya 40 na mshambuliaji mzawa, Abdulrahman Al-Oboud dakika ya 47.
    Timu hiyo ya Jeddah ina nafasi ya kushinda taji lingine msimu huu itakapokutana na Al Qadsiah katika Fainali ya Kombe la Mfalme ‘King’s Cup’ Mei 30.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AL ITTIHAD YA BENZEMA YATWAA UBINGWA LIGI YA SAUDIA ARABIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top