• HABARI MPYA

    Thursday, May 01, 2025

    HATIMAYE MBEYA CITY NAYO YAREJEA LIGI KUU


    KLABU ya Mbeya City imefanikiwa kurejea Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Cosmopolitan ya Dar es Salaam jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Mabao ya Mbeya City leo yamefungwa na Riffat Msuya dakika ya 16 na 28, Eliud Ambokile dakika ya 40, Faraji Kilaza Mazoea dakika ya 59 na David Mwasa dakika ya 70.
    Kwa ushindi huo,Mbeya City inafikisha pointi 65 na inakamilisha idadi ya timu mbili za kupanda baada ya Mtibwa Sugar yenye pointi 68 kufuatia timu zote kucheza mechi 29.
    Mbeya City inarejea Ligi Kuu baada ya misimu mitatu tangu ishuke daraja msimu wa 2021-2022 kufuatia kupanda kwa mara ya kwanza msimu wa 2013-2014.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HATIMAYE MBEYA CITY NAYO YAREJEA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top