• HABARI MPYA

    Monday, May 05, 2025

    SIMBA SC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI MECHI ZA VIPORO


    TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
    Bao pekee la Wekundu wa Msimbazi leo limefungwa na kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Fabrice Luamba Ngoma dakika ya 45’+6 akimalizia pasi ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda, Steven Dese Mukwala.
    Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 63 katika mchezo wa 24 ingawa inabaki nafasi ya pili nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 70 za mechi 26.
    Kwa upande wao JKT Tanzania baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 32 za mechi 27 sasa nafasi ya saba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI MECHI ZA VIPORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top