• HABARI MPYA

    Wednesday, May 21, 2025

    JKT QUEENS WATWAA UBINGWA WA LIGI YA WANAWAKE TZ BARA


    TIMU ya JKT Queens imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Gets Program jana Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
    JKT Queens imeipiku Simba Queens kwa wastani wa mabao tu (GD 62-42) baada ya timu zote kumaliza na pointi 47.
    Yanga Princess wamefanikiwa kumaliza nafasi ya tatu kwa pointi zao 39, Mashujaa Queens nafasi ya nne pointi 31 nafasi ya nne, Alliance Girls pointi 21 nafasi ya tano sawa na Ceasia Queens nafasi ya sita, tofuti wastani wa mabao GD -9 kwa -12.
    Nayo Fountain Gate Princess imemaliza na pointi 20 nafasi ya saba, Bunda Queens pointi 19 nafasi ya nane – huku Gets Program yenye pointi 10 na Mlandizi Queens ponti moja zikishuka daraja.
    MABINGWA LIGI YA WANAWAKE  
    2024 – 2025: JKT Queens
    2023 – 2024: Simba Queens
    2022 – 2023: JKT QUEENS
    2021 – 2022: Simba Queens
    2020 – 2021: Simba Queens
    2019 – 2020: Simba Queens
    2018 – 2019: JKT Queens
    2017 – 2018: JKT Queens
    2016 – 2017: Mlandizi Queens 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JKT QUEENS WATWAA UBINGWA WA LIGI YA WANAWAKE TZ BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top