MSHAMBULIAJI Mfaransa, Kylian Mbappé Lottin jana alifunga bao lake la 29 katika msimu wa La Liga, Real Madrid ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Sevilla Uwanja wa Ramón Sánchez Pizjuán Jijini Sevilla.
Mbappe alie katika msimu wake wa kwanza baada ya kuwasili kutoka Paris Saint-Germain alifunga bao hilo dakika ya 75 akimalizia pasi ya kiungo mkongwe Mcroatia, Luka Modrić – kabla ya kiungo wa Kimataifa wa England, Jude Bellingham kufunga bao la pili dakika ya 87 akimalizia pasi yamshambuliaji Gonzalo GarcÃa.
Mbappe anaendelea kuongoza kwa mabao yake 29, kati ya hayo saba amefunga kwa penalty akifuatiwa na mshambuliaji mkongwe wa Kimataifa wa Poland, Robert Lewandowski mwenye mabao 25.
Kwa ujumla Mbappe amekwishafunga mabao 40 katika mechi 54 za msimu wake huu wa kwanza Hispania baada ya kujiunga na Los Blancos – idadi ambayo inapitwa na Ronaldo Lima pekee aliyefunga mabao 47 akiwa Barcelona msimu wa 1996/1997.
Mbappe amefunga kwenye michuano mikubwa, mbali na mabao 29 ya La Liga, amefunga mengine saba katika Champions League, mawili Copa del Rey na kwenye Super Cup za Hispania na UEFA zote amefunga bao moja moja huku lingne moja akifunga kwenye Intercontinental Cup.
Real Madrid haina cha kujivunia msimu huu kufuatia kudondosha mataji yote kwa Barcelona ambao pia ni washindi wa El Clasico zote nne za msimu huu.
Nao mabingwa Barcelona jana walichapwa mabao 3-2 na Villarreal katika mchezo mwingine wa La Liga Uwanja wa OlÃmpic LluÃs Companys Jijini Barcelona.
Mabao ya Villarreal yalifunga na Ayoze Pérez dakika ya nne, Santi Comesaña dakika ya 50 na Tajon Buchanan dakika ya 80, wakati ya Barcelona yalifungwa na Lamine Yamal dakika ya 38 na FermÃn López dakika ya 45'+5.

0 comments:
Post a Comment