BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imesema kwamba itaupangia tarehe nyingine mchezo wa marudiano ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baina ya mabingwa watetezi, Yanga na mahasimu wao, Simba ambao uliahirishwa Machi 8, mwaka huu.
Taarifa ya TBLB jioni ya leo imesema kwamba hatua hiyo inafuatia Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) kukataa kusikiliza kesi ya Yanga kutaka ipewe ushindi.
Mchezo huo uliingia mgogoro baada ya Simba kutishia kutoingiza timu Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ilidai kuzuiwa kufanya mazoezi Macho 7, siku moja kabla ya mechi kwa mujibu wa kanuni.
Bodi ya Ligi ilitangaza rasmi kuuahirisha mchezo huo mchana wa Machi 8, lakini wakikwenda uwanjani na kufanya mazoezi kabla ya kuondoka na baadaye kufungua kesi CAS.
Wakati hayo yakiendelea, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliitisha kikao na viongozi wa klabu zote, Bodi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ingawa haikuwahi kutoa majibu yoyote juu ya mkutano huo uliohudhuriwa pia na viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
0 comments:
Post a Comment