• HABARI MPYA

    Thursday, May 29, 2025

    CHELSEA WATWAA UEFA CONFERENCE LEAGUE, WALITOKA NYUMA NA KUICHAPA REAL BETIS 4-1


    TIMU ya Chelsea FC ya England jana imefanikiwa kutwaa taji la UEFA Conference League baada ya kutoka nyuma 1-0 na kushinda 4-1 dhidi ya Real Betis Balompié ya Hispania katika mchezo wa Fainali Uwanja wa Tarczyński Arena mjini Wrocław nchini Poland.
    Pongezi kwa kocha Mtaliano, Enzo Maresca aliyewaongoza vijana wake kwa mbinu mbadala kipindi cha pili baada ya kutanguliwa kwa bao la mshambuliaji Mmorocco, Abdessamad Ezzalzouli dakika ya tisa.
    Mabao ya The Blues yalifungwa na kiungo Muargentina, Enzo Fernández dakika ya 65 na washambuliaji Nicolas Jackson wa England dakika ya 70, Jadon Sancho wa England dakika ya 83 na kiungo mwingine, Moisés Caicedo wa Ecuador dakika ya 90'+1.
    Hilo linakuwa taji la kwanza katika zama mmiliki mpya, Todd Boehly-Clearlake na Kocha Maresca pia aliyejiunga na timu mwanzoni mwa msimu.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA WATWAA UEFA CONFERENCE LEAGUE, WALITOKA NYUMA NA KUICHAPA REAL BETIS 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top