• HABARI MPYA

    Thursday, May 22, 2025

    RAIS DK MWINYI AWALIPIA SIMBA GHARAMA ZA UWANJA WA AMAAN


    RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi ametoa gharama zote za Uwanja wa New Amaan Complex, Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
    Mchezo huo wa marudiano utafanyika Jumapili kuanzia Saa 10:00 jioni — Simba SC wakimenyana na RSB Berkane ya Morocco.
    Simba inatakiwa kushinda mabao 3-0 baada ya kufungwa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi iliyopita Uwanja wa Manispaa ya Berkane mjini Berkane nchini Morocco.
    Tofauti na hivyo washinde 2-0 na mchezo uhamie kwenye dakika 30 za nyongeza hadi mikwaju ya penalti kusaka bingwa mpya wa taji hilo lilioachwa wazi na Zamalek ya Misri. 




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS DK MWINYI AWALIPIA SIMBA GHARAMA ZA UWANJA WA AMAAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top