• HABARI MPYA

    Wednesday, May 07, 2025

    NGORONGORO HEROES YATUPWA NJE AFCON U20


    TANZANIA imetupwa nje Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya Umri wa miaka 20 (AFCON U20) baada ya kufungwa bao 1-0 usiku wa jana na Zambia katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Suez Canal mjini Ismailia nchini Misri.
    Bao pekee la Junior Chipolpolo lililoizamisha Ngorongoro Heroes jana lilifungwa na kiungo wa FC Zurich ya Uswisi, Joseph Sabobo Banda kwa penalti dakika ya 90'+11.
    Hicho kinakuwa kipigo cha tatu mfululizo kwa Ngorogoro Heroes baada ya kuchapwa 1-0 mara mbili awali na Afrika Kusini na Sierra Leone — hivyo kupoteza nafasi ya kufuzu Robo Fainali kwa namba yoyote.
    Ushindi wa Zambia unaamsha matumaini kwao kufuzu Robo Fainali ikifikisha pointi tano katika nafasi ya tatu nyuma ya Afrika Kusini yenye pointi sita na Sierra Leone pointi saba, wakati Tanzania ambayo haina pointi inashika mkia nyuma ya wenyeji, Misri wenye pointi nne.
    Tanzania inakamilisha mechi zake za Kundi A Ijumaa kwa kumenyana na wenyeji, Misri.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGORONGORO HEROES YATUPWA NJE AFCON U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top