• HABARI MPYA

    Tuesday, May 20, 2025

    SERIKALI KUJENGA VIWANJA VITATU VYA MICHEZO MALYA


    WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasssim Majaliwa amesema Serikali imekusudia kukifanyia maboresho makubwa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya pamoja na ujenzi wa Akademi ya Michezo ambayo yanagharimu zaidi ya Bilioni 32.
    Mhe. Majaliwa amesema hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa majengo mbalimbali katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya mkoani Mwanza juzi (Mei 18, 2025).
    Amesema ujenzi huo mbali na majengo mengine ya shughuli za michezo utahusisha viwanja vitatu ambavyo vitakuwa na hadhi ya kuchezewa na timu yoyote ile.
    Aidha, amewataka wakazi wa Malya kutumia fursa hii kujiingizia kipato kwa kujenga vitega uchumi kwakuwa baadhi ya timu kubwa zitakuwa zinapiga kambi hapo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERIKALI KUJENGA VIWANJA VITATU VYA MICHEZO MALYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top