• HABARI MPYA

    Saturday, May 03, 2025

    NGORONGORO HEROES YACHAPWA TENA 1-0 NA SIERRA LEONE AFCON U20


    TANZANIA imepoteza mechi ya pili mfululizo ya Kundi lake, A Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (AFCON U20) baada ya kuchapwa 1-0 na Sierra Leone jioni leo Uwanja wa Suez Canal mjini Ismailia nchini Misri inakofanyika michuano hiyo.
    Bao pekee la Shooting Stars lililoizamisha Ngorongoro Heroes leo limefungwa na mshambuliaji wa Old Edwardians FC ya Ligi Kuu ya kwao, Samuel Armanki Gandidakika ya 37.
    Huo unakuwa mchezo wa pili kwa Ngorongoro Heroes iliyo chini ya Kocha mkongwe, Charles Boniface Mkwasa kupoteza baada ya kuchapwa 1-0 na Afrika Kusini Aprili 30 bao la Amajita likifungwa na kiingo wa Stellenbosch ya Ligi Kuu ya kwao pia  dakika ya 27 hapo hapo Suez Canal.
    Ngorongoro Heroes ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza Fainali za AFCON U20 - itashuka tena dimbani Jumanne kumenyana na Zambia, kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi A Ijumaa kwa kumenyana na wenyeji, Misri. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGORONGORO HEROES YACHAPWA TENA 1-0 NA SIERRA LEONE AFCON U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top